Mvutano wa CD wakwamisha kesi ya Zitto

Jumanne , 3rd Dec , 2019

Kesi ya uchochezi inayomkabili kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, imeshindwa kuendelea kusikilizwa leo Desemba 3, 2019, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kuibuka mzozo wa kutazama mkanda wa Video (CD), iliyokuwa ikionesha ushahidi dhidi ya mashtaka yake.

Kiongo Mkuu wa ACT Wazalendo, akiwa mahakani.

Kesi hiyo namba 327 ya mwaka 2018, ilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa, ambapo ulitokea mvutano wa Mawakili juu ya Hakimu kupokea ama kutokupokea ushahidi wa CD ili kusikia maneno aliyoyaongea Mbunge Zitto, wakati wa mkutano wake na Waandishi wa Habari, hali iliyopelekea kesi hiyo kuahirishwa hadi Desemba 4, 2019.

Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi, anayodaiwa kuyatenda Oktoba 28, 2018, katika mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika makao makuu ya ofisi za chama hicho zilizopo Kijitonyama, Jijini Dar es Salaam.