Moja ya majengo katika hospitali ya Taifa Muhimbili
Idadi hiyo imeongezeka ikilinganishwa na wagonjwa 23,989 waliopimwa Desemba 2014 hadi Oktoba 2015.
Takwimu hizo zimetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bw. Aminiel Aligaisha wakati akitoa mafanikio ya hospitali hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja wa awamu ya tano ya utawala wa Dkt. John Pombe Magufuli na kuongeza kuwa hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 129.57.
Kwa upande wa mapato ya hospitali hiyo kwa sasa wanaingiza shilingi bilioni 4.6 kwa mwezi kutoka wastani wa shilingi bilioni 2.3 kwa mwezi katika siku za nyuma.
Aidha, ameongeza kuwa hospitali hiyo imeshaanza harakati za kuweka huduma za kupandikiza figo kwa wagonjwa na ifikapo mwezi wa kwanza 2017 huduma hiyo itaanza kutolewa nchini na wataalam tayari wamepelekwa nchini India kwa mafunzo zaidi.
