Alhamisi , 19th Mar , 2020

Msanii wa muziki wa Hip Hop hapa nchini Mwana FA, amekutwa na maambukizi ya homa kali inayosababishwa na virusi vya Corona na kwamba amewekwa karantini na kwa sasa anaendelea vizuri.

Msanii wa muziki wa Hip Hop Mwana FA.

Kupitia video yake iliyoiweka kwenye mitandao ya kijamii, Mwana Fa amesema kuwa majibu ya vipimo vya sampuli amepatiwa leo Machi 19, 2020, na hali alinayo kwa sasa si kama ile aliyokuwa nayo juzi wakati akirejea nchini kutokea Afrika ya Kusini na kuwataka Watanzania kuzingatia tahadhari zinazotolewa.

"Nilivyorudi nikajitenga ili kuhakikisha siambukizi wengine, ugonjwa huo unaweza ukampata mtu yoyote na homa niliyokuwa nayo juzi haipo tena kwa sasa nipo shwari, tujihadhari tu, COVID-19 si ugonjwa wa kutisha sana, kwa sababu tumekuwa tukipata magonjwa mabishi zaidi ya hii" amesema Mwana FA.