
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Kauli hiyo ameitoa leo Machi 15, 2021, wakati akizungumza na wananchi wa Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga ikiwa ni sehemu yake ya ziara ndani ya mkoa huo iliyoanza hii leo.
"Tanzania tupo salama ni kawaida ya mwanadamu kukaguliwa kaguliwa mara mafua mara homa mara hiki, lakini nataka niwaambie kwamba katika wakati muhimu wa Tanzania kushikamana ni wakati huu, kujenga umoja ni wakati huu siyo wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje yakatuparaganya vichwa," amesema Mhe. Samia.