Mwanafunzi ampa mimba mwanafunzi mwenzake

Jumanne , 3rd Dec , 2019

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Songwe, imempandisha kizimbani Chrispin kibona (18) mwanafunzi wa kidato Cha pili Idigima Sekondari, kwa tuhuma za kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake miaka wa 17.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Songwe.

Akisomewa mashitaka hayo Mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka wa Serikali Gibson Tawale mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Neemes Chami, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Januari 19, 2019, saa sita mchana, katika kijiji cha Iyula Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, ambapo alimbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake wa kidAto cha pili mwenye umri wa miaka 17.

Aidha Mwendesha mashita wa Serikali Gibson ameongeza kuwa aliyepewa ujauzito na alimpatia wote walikuwa wanafunzi wa Shule Sekondari Idigima kidato cha pili, ambapo upelelezi wa tukio hilo umekaamilika.

Kwa upande wake mtuhumiwa huyo wa ubakaji mwenye umri wa miaka 18 amekana shitaka hilo na Hakimu wa Mahakama hiyo Neemes Chami, amehairisha hadi tarehe 10 mwezi wa 12 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa tena.