Ijumaa , 17th Jul , 2015

Zoezi la kuchukua fomu za ubunge na udiwani kwa wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) limeendelea leo kwa siku ya pili ambapo wagombea wameahidi kuleta maendeleo ikiwa watapitishwa na chama.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia chama cha (CCM) Bw. Frank Kibiki.

Mgombea wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia chama cha (CCM) Bw. Frank Kibiki amesema ikiwa atapitishwa na chama chake atashirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo.

Bw. Kibiki amesema jimbo la Iringa linahitaji mbunge ambaye anatambua matatizo ya wananchi na jinsi ya kuyatatua.

Zoezi la kuchukua fomu za kugombea ubunge na udiwani limeanza Julai 15 na linatarajia kukamilika Julai 31, na wananchi watawapigia kura ya maoni wagombea Agosti Mosi mwaka huu.