Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mwanamke amtupa mtoto ziwani

Jumatano , 14th Jun , 2017

Mwanamke mmoja mkazi wa Kisiwa cha Nyamango anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miezi saba baada ya kumtupa ziwa Victoria.

DCP Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Nyamisi Bahati (27) anayedaiwa kumuua mtoto wake aitwaye Sakimu Hassani baada ya kumtupa ziwa Victoria na kupelekea mtoto huyo kupoteza maisha, tukio analodaiwa kulifanya majira ya saa 1:00 usiku ya tarehe 13/06/ 2017.

Inadaiwa mtuhumiwa ambaye ni mama wa mtoto huyo alitoka nyumbani kwa mumewe na kwenda kuwasalimia wazazi wake akiwa na mtoto wake, lakini baadaye alitoka nje akiwa na mtoto kama anakwenda kumbembeleza ndipo baada ya muda kupita alirudi akiwa hana mtoto na kupelekea Mama yake mzazi wa binti huyo kumuuliza mtoto amemuweka wapi ndipo mtuhumiwa alionekana na mashaka huku akishindwa kuonyesha mahali mtoto alipo na baadaye akasema amemtupa kwenye Ziwa Victoria.

Kamanda Msangi amesema baada ya mtuhumiwa kusema hivyo, Bibi wa mtoto alipiga yowe akiomba msaada kwa watu ili waweze kuja kumuokoa mtoto na wananchi walipofika waliweza kutoa taarifa kituo cha Polisi na kuweza kufika eneo la tukio ambapo walishirikiana na wananchi na kufanya kazi ya kumtafuta majini na baadaye walifanikiwa kumpata ila alikuwa tayari ameshapoteza maisha.

Kamanda Msangi ameendelea kusema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha mtuhumiwa wa mauaji hayo anasumbuliwa na matatizo ya akili, japokuwa Polisi wapo katika upelelezi na mahojiano na mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

 

 

 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa