Jumatano , 2nd Feb , 2022

Jeshi la Polisi mkoa wa Geita linaendelea na uchunguzi kufuatia tukio la mauaji ya mke wa mfanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa GGM, aliyekutwa amenyongwa nyumbani kwake jana Februari Mosi, 2022, majira ya saa 8:00 mchana.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe

Taarifa ya mauaji hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe na kusema tukio hilo limetokea mtaa wa Majengo, Kata ya Kanyara, halmashauri ya mji Geita, ambapo mwanamke huyo aitwaye Anjela Anteli (43), alikutwa amenyongwa.

Kamanda Mwaibambe, amesema kuwa mtu wa kwanza kugundua alikuwa bodaboda ambaye aliagizwa kupeleka maziwa nyumbani hapo na alipofika akagonga mlango bila mafanikio.