Jumanne , 23rd Feb , 2016

Hospitali ya rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es salaam inakabiliwa na msongamano mkubwa wa chumba cha kuhifadhi maiti, hali iliyochangiwa na kutokuwepo

Hali hiyo inaelezwa kuwa ni kutokana na kukosekana kwa vyumba vya kuhifadhia maiti katika hospitali zilizopo manispaa ya Kinondoni na kupelekea maiti nyingi kupelekwa chumba cha maiti katika hospitali hiyo.

Akielezea changamoto hizo kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Mwananyamala Delila Moshi amesema kuwa mbali na changamoto hiyo kuna tatizo kubwa la hospitali kupokea idadi kubwa ya wagonjwa tofauti na makadirio.

Amesema kuwa uwezo wa hospitali ilikuwa kuhudumia wagonjwa 500 kwa siku lakini hivi sasa wanahudumia wagonjwa zaidi ya 1500 kwa siku.

Aidha miundombinu ya hospitali hiyo na watumishi waliopo hawakidhi mahitaji halisi huku kukiwa na upungufu mkubwa wa mashuka kwaajili ya wagonjwa.

Amesema mahitaji ni mashuka 2114 lakini mashuka yaliyopo ni 402 pekee hivyo anawaomba wahisani watakaoguswa kujitokeza kutatua changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.