Jumanne , 21st Feb , 2023

Watu watano wa familia moja wamenusurika kifo baada ya watu wasiojulikana kuchoma milango na madirisha ya nyumba ya Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Ilola Halmashauri ya Shinyanga usiku wa manane wakati wakiwa wamelala na kutokomea kusikojulikana.

Nyumba iliyofanyiwa jaribio la kutaka kuchomwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi, amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi kati ya mtumishi huyo na mume wake.

Moto huo ulianza kuwaka majira ya saa 8:00 usiku wakati wakiwa wamelala baada ya watu wasiojulikana kuchoma moto nyumba ya mtumishi huyo aitwaye Bandi Magoye, huku tukio hilo likihusishwa na ugomvi wa wanandoa hao ambao walishatengana na talaka imeshatolewa mahakamani, huku jeshi la polisi likimshikilia mzazi mwenzie na mwanamke huyo.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Ihalo, Kata ya Ilola wamesema walipata taarifa ya tukio hilo usiku na kwenda kutoa msaada ambapo walikuta moto umezimwa na watu waliokuwa ndani wote wakiwa salama.