Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mzee wa Upako afunguka kuhusu yeye kunywa pombe

Jumapili , 19th Feb , 2017

Mchungaji Anthony Lusekelo amefunguka kuhusu tuhuma za yeye kunywa pombe, na kuweka wazi kuwa hanywi pombe bali anakunywa 'wine' isiyo na kilevi, huku akisita kusema endapo unywaji pombe ni dhambi au siyo dhambi.

Mch. Anthony Lusekelo

Amefunguka hilo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI cha EATV, na kuweka wazi kuwa wanaomtuhumu kuwa yeye anakunywa pombe wanapaswa kutoa ushahidi juu ya tuhuma hizo, na kwamba unywaji pombe unaweza kuwa dhambi ama usiwe dhambi kulingana na imani na dini ya mtu.

"Hao wanaotuhumu kuwa nakunywa pombe, waeleze ni pombe gani nakunywa, nilikuwa nakuywa wapi na aliyeniona ni nani... kuna sehemu nyingine pombe siyo dhambi, dini nyingine mpaka kanisani kuna bar".

Je, kunywa bia kiasi bila kulewa ni dhambi au siyo dhambi?

Hilo ni swali lingine alilokutana nalo kuhusu unywaji Pombe, ambapo katika majibu yake amesema hawezi kusema kama ni dhambi au lah, maana inategemea na imani ya mtu, huku akiongeza kuwa Bibilia haijazuia unywaji pombe

"Inategemea na makanisa, kuna mengine hata kunywa soda ni dhambi. Dhambi ni makubaliano yenu kwenye dini yenu. Bibilia inasema kula kitu chochote hata chakula kama ukila kupitiliza ni dhambi, hata unywaji wa pombe ukinywa ukapitiliza ni dhambi. Biliblia haijaandika moja kwa moja kwamba msinywe pombe, imesema msilewe kwa kuwa ndani ya ulevi kuna ufisadi, cha msingi mbadilishe ulevi wenu uwe ni roho mtakatifu"

Ikumbukwe kuwa sekeseke lililosababisha Mzee wa upako adawe kunywa pombe, lilihusisha kurushiana mane na jirani zake ambapo baada ya hapo vyombo vya habari hasa magazeti yaliripoti tukio hilo kwa namna ambayo Mzee wa Upako hakuipenda, na hata kufikia hatua ya kuwatabiria kifo waandishi walioandika habari hiyo.

Alipoulizwa kuhusiana na ahadi yake hiyo ya kuwatabiria vifo, alisema kuwa tayari amewasamehe ingawa uwezo wa kuwaombea kifo anao.

"Tulisema hatuwezi kutumia nguvu kubwa sana kuwaombea watu kifo, kwa sababu sisi ni wanadamu, na wanadamu tuna mapungufu kwahiyo nikaona ni bora kumuachia Mungu. Uwezo huo wa kuwaombea watu wakafa, mimi ninao, lakini nikaona inasaidia nini mtu kumuombea mabaya, kwahiyo nikaamua kusamehe"

Baadhi ya watu walitaka kujua ni kwanini haendi kuombea wagonjwa hospitalini ili wapone, ambapo alijibu kuwa maombi hufanywa katika mazingira maalum, na kwamba hospitali kila mgonjwa ana imani yake.

"Maombi lazima kuandaa mazingira, na sehemu ambayo Mungu amesema tukutane ni kanisani, ndiyo maana hata wakati wa Yesu wagonjwa ndiyo walimfuata Yesu, siyo Yesu aliwafuata wagonjwa.. Kinachoponya ni imani ya mtu, pale hospitali kila mtu ana imani yake, wakati mwingine hata kumuombea mtu inabidi umuombe kwanza maana wengine hawapendi kuombewa"

Tazama hapa sehemu ya kipindi cha Kikaangoni akianza kujibu swali kuhusu wale aliowatabiria kifo.....

HABARI ZAIDI

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa