Dkt. Doto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.
Mbali na utendaji mbovu, wizi fedha za umma ndani ya Shirika pamoja na wizi wa vifaa vya umeme uliokithiri umetajwa pia kama miongoni mwa sababu zilizopelekea bodi hiyo kuvunjwa.
Dkt. Biteko ametoa agizo hilo wakati wa Kikao kazi baina yake na Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kampuni zake tanzu, Wakurugenzi wa TANESCO wa Kanda na Mameneja wa Mikoa ambacho kimefanyika tarehe 28 Machi, 2024 jijini Mwanza kikiwa na lengo la kujadili utendaji kazi katika Sekta ya umeme.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Bodi ya TANESCO kuagizwa kumuondoa Meneja Mkuu wa ETDCO kutokana na utendaji mbovu wa kazi ndani ya Taasisi na kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya umeme ukiwemo wa usafirishaji umeme kutoka Tabora hadi Urambo na Tabora hadi Mpanda.
Dkt. Biteko ameagiza Watumishi wote wanaojihusisha na wizi ndani ya Shirika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria ikiwemo kuwaweka pembeni katika Utumishi maana wao ni sababu ya watanzania kutokupata umeme wa uhakika
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amewataka watendaji wa TANESCO kujirekebisha wao wenyewe na wasisubiri kurekebishwa kwani yapo maeneo ambayo wanaweza kusimamia bila kusubiri viongozi ikiwemo kuwafanya watumishi walio chini kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi.
Pia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio ameweka msisitizo kwa Watendaji wa TANESCO kuwa lazima wabadilishe taswira ya Shirika hilo kwa wananchi kwa kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora.
Baadhi ya Watendaji wa TANESCO kwenye kikao hicho wamekiri kuwa taswira ya Shirika hilo kwa wananchi bado inahitaji kuboreshwa ili kuweza kuaminika zaidi kwa wananchi ikiwemo taarifa mbalimbali zinazotolewa na Shirika hilo.