Jumamosi , 16th Oct , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amemuahidi Askofu Shoo kwamba atahakikisha anaendelea kuwahudumia Watanzania na kuwatazama kwa jicho la huruma kama lilivyo jicho lake huku akiomba aombewe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 16, 2021, wakati aliposhiriki maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya Hospitali ya KCMC.

"Nitaendelea kuhudumia Watanzania kwa jinsi na kadri Mungu atakavyoniwezesha, nitaendelea kuwatazama Watanzania kwa jicho la huruma kama lilivyo jicho langu na jinsi Mungu atakavyoniwezesha, naomba mniombee na mnipe ushirikiano mkubwa ili kazi ya kuendesha Taifa hili iwe rahisi kwangu," amesema Rais Samia