Alhamisi , 10th Feb , 2022

Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, ametoa leseni za kuanza kuchapishwa tena magazeti ya MwanaHALISI, Mawio, Mseto na Tanzania Daima.

Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye

Leseni hizo amezikabidhi hii leo Februari 10, 2022, wakati akikabidhi leseni katika kikao na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

"Leo nitatoa leseni kwa magazeti manne yaliyokuwa yamefungiwa kwa sababu ni vizuri kuondoka kwenye maneno tutende si ndiyo, hivyo tuanze na ukurasa upya sasa mwenye maneno yake aseme mwenyewe, kifungo kimetosha, kikubwa kazi iendelee," amesema Waziri Nape