Jumanne , 7th Jun , 2016

Serikali imesema kuwa kutokana na baadhi ya wabunge wengi na baadhi ya viongozi wa kiserikali kutokuwa na uelewa juu ya sera ya ugatuaji madaraka wataanda semina kwa ajili ya wabunge wote ili kutoa elimu na kuondoa migongano ya kiutawala.

Waziri wa TAMISEMI, Mhe. George Simbachawene.

Akiongea Bungeni leo Mjini Dodoma Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. George Simbachawene, amesema kuna malalamiko mengi yanatokea katika Halmashauri juu ya uendeshaji wa kutokana na kuona kuna muingiliano wa kiutendaji na viongozi wa serikali wakiwemo wa wakuu wa mikoa na Wilaya.

Mhe. Simbachawene amesema kutokana na jambo hilo la ugatuaji madaraka kukaa kwa mujibu wa Katiba viongozi wengi wanaamini kuwa kuna muingiliano mkubwa katika utoaji maamuzi hali inayopelekea halmashauri nyingine kuwa na sintofahamu juu ya viongozi wakuu wa serikali.

Akitolea ufafanunuzi juu ya suala la kufutwa kwa wenyeviti wa serikali za mitaa na jambo hilo lifanywe na wakuu wa wilaya na mikoa amesema watedaji hao wakuu wa serikali hawana haki ya kuingilia masuala ya utendaji katika mitaa zaidi ya kusimamia shughuli za kiutendaji kama zinakwenda vizuri na zinafuata sheria na taratibu za nchi na maagizo mbalimbali ya serikali kuu.

Sauti ya Waziri wa TAMISEMI, Mhe. George Simbachawene