Jumatatu , 12th Nov , 2018

Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amegusia suala la korosho kwenye mkutanowa 13 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati kwenye mkutano wa Jumatatu novemba 12 akiuliza swali kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye

Katika kikao hicho Nape Nnauye aliuliza "katika jitihada za Mkoa wa Lindi kuboresha elimu tulipitisha kila kilo moja ya korosho kukatwa shilingi 30 ili kuboresha elimu, kwa halmashauri kama ya kwangu tulipata zaidi ya milioni 400, Nini mpango wa serikali kuendeleza mpango huu, kwa kuwa wote tunajua hali iliyotokea kwenye korosho, ile fedha hatuwezi kuipata tena?".

Akijibu swali hilo ni vizuri Naibu Waziri TAMISEMI, Josephat Kandege amesema "Nape tusubiri najua unatamani korosho zinunuliwe, lakini vile ambavyo tulipanga viende kwenye maendeleo lazima viendelee,"

Kumekuwa na sintofahamu juu ya ununuzi wa zao la korosho baina ya wakulima, serikali pamoja na wafanyabiashara hali iliyopelekea serikali kutoa siku 4 kuanzia Ijumaa ya wiki iliyopita hadi leo jumatatu ya novemba 12 saa 19 jioni kama watanunua au hawatanunua.

Akizungumza na wanajeshi pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa nchini ambapo aliambatana na Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Venance Mabeyo amesema "tumejifunza wametupa akili mapema wamechelewa na korosho zetu tutaziuza, na msimamo huu pia utaendelea kwenye mazao mengine kwa wale watakaotaka kuchezea wakulima, lazima tujipange kikamilifu."