Jumatano , 14th Aug , 2019

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekanusha habari iliyosambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii ikieleza taasisi hiyo kukiri sekta ya ajira binafsi kupungua kwa asilimia 42.6% na serikalini zikiwa mepungua kwa asilimia 78.1% ndani ya mwaka mmoja.

Katika taarifa hiyo, NBS imesema kuwa wanajiandaa kufanya utafiti wa watu wenye uwezo  wa kufanya kazi utakaofanyika mwaka 2019/20 na ilifanya makisio ya mwenendo wa hali ya soko la ajira kwa 2018.

"Matokeo ya takwimu hizo yanaonesha kuwa idadi ya watu walio na ajira imeongezeka kutoka milioni 20.0 mwaka 2014 hadi milioni 22.0 mwaka 2018", imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Takwimu hizi hutumika pia kama kigezo cha kufanya maoteo ya hali ya ajira katika vipindi ambavyo hakuna tafiti zilizofanyika ili kutoa hali ya soko la ajira katika vipindi vifupi vifupi.

"2017/18 kulikuwa na jumla ya ajira 552,063 zilizozalishwa nchini ikilinganishwa na ajira 453,466 kwa mwaka  2016/17, hili  ni  ongezeko la  ajira  98,597  sawa  na  asilimia  21.7  kati  ya  mwaka 2016/17 na mwaka 2017/18."

Aidha NBS imefafanua kuwa kati ya ajira 552,063 zilizozalishwa nchini mwaka 2017/18, ajira 415,009 sawa na asilimia 75.0  zilikuwa  ni  ajira  kutoka  Serikalini, ajira hizi zinajumuisha ajira 18,000 kutoka Serikali Kuu  na  ajira  397,009 kutoka  katika  miradi  ya  maendeleo  kupitia  Mpango  wa  Pili  wa Maendeleo wa Taifa wa m