Jumatatu , 18th Mei , 2020

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, amehoji kama ipo sababu ya wananchi kuendelea kuwapigia kura na kuwachagua viongozi wa CHADEMA, kwa kile alichokieleza kuwa chama hicho ni kama kundi tu ambalo linaongozwa na mtu mmoja.

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai.

Spika Ndugai ameyabainisha hayo leo Mei 18, 2020, jijini Dodoma, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kumuomba Mbowe ajirekebishe kwa kuwa amekuwa ni kiongozi kwa muda mrefu na aache kuwaonea Wabunge wake ikiwemo kuwakata mishahara yao.

"Wabunge wamechaguliwa na wananchi, wewe unawafukuza tu, haujali hata wale wananchi waliokaa foleni kuwachagua wawakilishi wao, hivi kesho na keshokutwa mwananchi ana sababu gani ya kuchagua Mbunge wa CHADEMA, ambaye anaenda kutawaliwa na Mbowe na kundi lake na kuamrishwa mwanzo mwisho, kuingizwa na kutolewa Bungeni wanavyotaka wao, Mbowe ajifunze kubadilika" amesena Spika Ndugai.

Aidha Spika Ndugai, amemuomba Mbowe kuacha kujipima mabavu na Rais Magufuli kwa kuwa ni mkuu wa nchi na anapaswa kumuheshimu.