
Waziri mkuu wa zamani wa Israel Benjamin Netanyahu
Uchaguzi wa leo unafanyika baada ya serikali ya muungano wa mageuzi uliovileta pamoja vyama vinane kusambaratika. Vyama hivyo vilifanikiwa kumuondoa madarakani Netanyahu lakini vikashindwa kuleta uthabiti wa kisiasa.
Waisraeli wana muda hadi saa mbili usiku saa za Israel kupiga kura na baadaye mchakato wa kuunda serikali ya mseto utaanza.
Waziri Mkuu aliye madarakani Yair Lapid anataka kuendelea kushikilia madaraka, huku chama chake cha Yeish Atid kikiwa nyuma ya chama cha Likud cha Netanyahu katika kura za maoni.
Lapid amewahimiza Waisraeli wajitokeza kupiga kura vizuri kwa mustakabali wa watoto wao na taifa lao.