Jumatano , 11th Dec , 2019

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt Athman Ngenya, amesema kuwa licha ya Shirika hilo kujitahidi kukomesha uingizwaji wa nguo za ndani zisizotakiwa, lakini bado nguo hizo zimekuwa zikiendelea kuuzwa kila kukicha.

Nguo za ndani za Kike.

Dkt Ngenya ameyabainisha hayo leo Desemba 11, 2019, wakati akitoa tathimini ya mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya Tano.

"Nikiri kwamba nguo za ndani zinatupa changamoto, tunajitahidi sana kuhakikisha hazipo lakini kila ukipita Manzese unakuta zinaning'inia, sasa wafanyakazi wa TBS nchi nzima wako 478 na tuna majukumu mengi, tunamikakati kwa Nchi nzima kuhakikisha tunakomesha uingizwaji wa bidhaa zisizokidhi viwango" amesema Dkt Ngenya.

Aidha Dkt Ngenya ameongeza kuwa katika kuhakikisha Shirika hilo linaboresha huduma zake, limefanikiwa kutumia kiasi cha shilingi bilioni 20 katika ujenzi wa jengo lake jipya la maabara lenye ghorofa nane.