Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na Mkurugenzi wa NIDA Andrew Massawe mapema leo Jijini Dar es salaam.
Mkakati huo umetangazwa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba alipokutana na uongozi na wafanyakazi wa NIDA, kwa lengo la kujadili mikakati mbalimbali ya kuboresha utendaji wa mamlaka hiyo.
Amesema tayari serikali imekamilisha kanzidata ya wananchi walizozipata kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC na kwamba, tayari taasisi zaidi ya 35 zimeanza kutumia taarifa za NIDA katika kufanya utambuzi wa wafanyakazi wao sawia na kupunguza usumbufu kwa wananchi kuhusu taarifa zinazowahusu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa NIDA Bw. Andrew Massawe amesema kwa zoezi la awali lililofanyika nchi nzima tayari wamefanya uhakiki wa kuwatambua watumishi wa serikali takribani laki tano na elfu sitini na tano.


