Jumatano , 23rd Nov , 2022

Noti mpya zinazinduliwa nchini Nigeria leo katika juhudi za kupambana na makundi ya kihalifu  na ufadhili wa makundi ya Kiislamu na watekaji nyara.

Inatarajiwa kuanzishwa kwa noti mpya za naira 200, 500 na 1,000 kutasaidia kuongeza sarafu ya ziada katika mzunguko na kupunguza mfumuko wa bei.

Genge moja la utekaji nyara tayari limejibu uzinduzi wa sarafu hiyo mpya.

Genge hilo limepunguza nusu ya mahitaji yao ya fidia kwa watu wazima wawili na watoto wawili waliokamatwa katika jimbo la Zamfara, wakisisitiza kuwa inalipwa katika noti mpya kabisa.