Jumatatu , 14th Sep , 2020

Mgombea Urais kupitia CCM Dkt John Magufuli, leo Septemba 14, 2020, amesema kuwa kila anapomfikiria Hayati Benjamini William Mkapa, moyo unamuuma kwa kuwa ndiye aliyemuona na kumnadi kuwa Mbunge wa Chato.

Mgombea Urais kupitia CCM, Dkt John Pombe Magufuli

Dkt Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo wakati akizungumza na wananchi wa Chato wakati wa mkutano wake wa kampeni na kuendelea kusisitiza suala la amani kwa Watanzania.

"Mzee Mkapa wakati ananinadi alininadi kwenye kiwanja hikihiki, ndiyo maana kila ninapomfikiria Mzee Mkapa moyo unaniuma, maana yeye ndiye aliyeniokota huku jalalani, kwa sababu kuna msemo siku hizi mtu akipata kazi anaitwa ameokotwa jalalani na Magufuli", amesema Dkt Magufuli.

Tazama video hapa chini