Nikki Mbishi aumizwa na Fid Q, amtaka wazikane

Alhamisi , 14th Mar , 2019

Rapa anayeamianika kwa kufanya vyema kwenye mitindo huru nchini, Nikki Mbishi amekiri kuhuzunishwa na Rapa mwenzake Fareed Kubanda 'Fid Q' kwa kugawa 'CD' yake kwa mtu baada ya yeye kumpatia.

Rapa Fid Q

Mbishi amesema kwamba kitendo cha Fid Q kumpatia mtu mwingine CD ambayo yeye alimpatia kimempa ukakasi kidogo  lakini ameona hakuna shida japo yeye amemchukulia poa.

"Sikuelewa maana ya kukupatia copy ya album yangu na wewe ukagawa kwa yule jamaa halafu bure tena kwa mtu ambaye hakuwa hata na interest, ni bora ningebaki na CD yangu, maana nilikupa kwa heshima ila nikaona umeichukulia poa", amesema Mbishi.

Hata hivyo baada ya Mbishi kuanika kuumizwa kwake hadharan,i Rapa Wakazi amekiri kwamba Fid q ni kweli amemkosea rapa huyo huku akimfafanulia jambo linaloweza kuwa sababu.

"Kutakuwa na sababu kubwa nyuma yake. Labda ulikuwa umemuudhi hapo nyuma, akawa ameshikilia hisia ngumu", amesema Wakazi.

Pamoja na hayo, Rapa Fid Q, amemjibu Mbishi kwenye sintofahamu hiyop na kusema kwamba "Yule niliyempa CD ni mdau na anamiliki radio sauzi, nilifanya vile baada ya kumtambulisha kwako na nia yangu (niliitamka huku unaisikia) nilitaka akusikie ili ajue wewe ni mahiri kiasi gani na kama kuna uwezekano wa dili basi akupe..ni hayo tu"