
Bongozozo
Ametembelea Bunge kwa mualiko maalum kujionea shughuli za uendeshaji ndani ya Bunge hilo na akizungumza baada ya kutoka Bungeni, Bongozozo amesema kuwa ametembea sehemu nyingi duniani lakini hakuwahi kutembelea sehemu muhimu kama Bunge.
"Mimi nasikia raha sana, sijawahi kutembelea Bunge lolote duniani. Mimi ni msafiri na ninapenda vitu vipya vipya, kwahiyo nilivyoingia pale nikaona raha kusikia watu wanaongea vitu vizito. Wanapeleka malalamiko yao kutoka vijijini", amesema Bongozozo.
"Nilipenda swali kutoka kwa mbunge mmoja mpaka nikataka kupiga kelele. Nilipouliza kuwa naweza kupiga kelele nikaambiwa hapana siruhusiwi lakini wao wanaruhusiwa. Swali lenyewe lilikuwa juu ya uraia pacha", ameongeza Bongozozo.
Akizungumzia kuhusu kupewa ubalozi na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla, Bongozozo amesema kuwa kilichomsaidia kupewa ubalozi huo ni ucheshi wake na kuongea sana.
"Wapo watu kule wanajitolea na wanayajua sana mambo haya lakini mimi nina kelele tu ndiyo maana nikapewa. Sema ninawapa sifa wale ambao wanajitolea kimyakimya pia", amesema.