Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Mstaafu Kikwete ameyasema hayo hivi karibuni wakati akizindua usomaji wa kwanza wa kitabu chake katika Chuo Kikuu cha Newyork kilichopo Marekani ambacho amekipa jina “The Journey of My Life From a Barefoot Schoolboy to President”.
Rais Kikwete amesema “Nilipata viatu (raba) kwa mara ya kwanza nilivyotoka jandoni ,nilikwenda navyo shule mwalimu akanambia kesho usije na viatu kila mtu hana viatu humu, kitu muhimu nachowashauri wazazi wawasaidie watoto wao kusoma, na watoto watimize wajibu wao wa kusoma".
Kitabu hicho kinatarajiwa kufanyiwa tafsiri ya kiswahili ikielezea maisha ya kiongozi huyo mstaafu ambae alishawahi kuiongoza Tanzania kama wa Rais wa awamu ya nne kuanzia mwaka 2005 hadi 2015 akiwa pia Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM).