Jumatatu , 26th Oct , 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema mara atakapostaafu nafasi hiyo ya juu ya uongozi mwaka huu anatarajia kuanzisha taasisi ya maendeleo Afrika na Dunia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipiga kura Jana

Rais Kikwete amesema hayo jana katika kijiji cha Msoga, Chalinze Wilayani Bagamoy Mkoani Pwani baada ya kupiga kura yake kwenye uchaguzi mkuu na kusema kuwa mara baada ya kustaafu atajihusisha na masuala ya Maendeleo.

Aidha Rais Kikwete amesema kuwa atarudi kijijini kwake Msoga ambapo mbali ya kuanzisha taasisi hiyo ya maendeleo pia ataendeleza ufugaji na kilimo cha mananasi.

Kuhusu Uchaguzi wa Mwaka huu raisi Kikwete amesema uchaguzi wa nyakati zote huwa na upinzani makali na liomba hali ya amani iendelee hiviv ili Tanzania iwe nchi ya mfano kwa kufanya uchaguzi bila kuwa na Vurugu.