Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

"Nitanunua kipindi kumsifu Rais" - Mch. Msigwa

Jumatatu , 9th Jul , 2018

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) ameweka bayana kwamba hahitaji kuviziwa na mtu yoyote katika suala la kusifu utendaji wa Rais Magufuli pamoja na serikali yake kwani ana uwezo wa kununua kipindi katika televisheni ili kuweza kufanya jambo hilo.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mch. Peter Msigwa

Akifanya mahojiano na www.eatv.tv, Msigwa amesema kwamba kitendo cha kusambaa kwa kipande cha 'video' kilichokuwa kikimuonyesha akimsifu Rais wakati alipokuwa kwenye ziara mkoani Iringa kilikuwa cha kuviziwa na
kilikuwa na lengo la kumchafua kisiasa.

Mbunge huyo wa upinzani amedai kwamba kitendo cha hali ya uchumi wa nchi kuwa mdogo, watu kuokotwa kwenye viroba na demokrasia kukandamizwa ndivyo vinamfanya kushindwa kutoa pongezi lakini siku akiona inahitajika, atafanya hivyo na siyo kuviziwa viziwa kama jinsi ilivyofanyika awali kupitia kipande cha 'video'.

"Hakuna wa kunizuia nikitaka kumpongeza Rais, hivyo sihitaji kuviziwa.  Mimi sikumpongeza Rais ile siku na simpongezi. Kilichofanyika naweza kusema 'I was taken out of context' Nina uwezo wa kununua kipindi ili kumsifia Rais ila si kwa kuviziwa viziwa," amesema Msigwa.

Akizungumzia kuhusu wakati mgumu alioupata ndani ya Chama chake na kwa wafuasi wanaoiunga mkono CHADEMA baada ya kusambaa kwa 'video' ile, Msigwa amesema haikuwa rahisi kueleweka na watu wote.

"Chama changu kinajua msimamo wangu, hivyo niliwaeleza wakanielewa. Watu wengine haikuwa rahisi  kunielewa kutokana na kale ka video cha sekunde 53 ambacho kalikatwa mwanzo na mwisho. Wasomi na watu wanaoniamini walielewa," ameongeza Mch. Msigwa.

Rais Magufuli akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Iringa, Mei 3, mwaka huu wakati kulisambaa 'video' inayomuonyesha Mch. Msigwa akimsifia Rais, ambapo kwa mujibu wake amesema ni kama aliviziwa kwani hata walipoingia ndani kuzungumza na Rais hawakuwa na vifaa vyao vya mawasiliano zaidi ya waandishi wa Ikulu.

HABARI ZAIDI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu

Mwili wa Boaz Sanga, Mwanafunzi wa CHuo cha SAUTI Mwanza baada ya kupatikana Pembezoni wa Ziwa Viktoria

Mwanafunzi wa SAUTI afariki akijaribu kuogelea

Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri, CDF Mpya wa Kenya

Luteni Charles Muriu ateuliwa kuwa CDF mpya Kenya

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa 124%

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita