Jumatatu , 4th Jul , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba wenye akili za kawaida wamekuwa wakilaumu yeye kwenda nje ya nchi badala ya kufanya ziara mikoani, na kusema anapoenda nje ya nchi huenda kutafuta fedha za maendeleo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ametoa kauli hiyo hii leo Julai 4, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati wa utiaji saini mkataba wa ujenzi wa kipande cha nne cha Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) Isaka-Tabora chenye thamani zaidi ya shilingi trilioni 2.

"Wale wenye akili za kawaida ni rahisi kulaumu Rais anasafiri tu, Rais hakai, badala ya kutembelea mikoa anatembelea tu nje, lakini matokeo yake ndio haya, nikienda mkoani nitajenga siasa ya ndani hakuna maendeleo, nikienda nje nakwenda kutafuta fedha hizi kwa ajili ya maendeleo,"amesema Rais Samia