Jumatano , 12th Oct , 2016

Rais Barack Obama awataka viongozi waandamizi wa chama cha Republican kujiondoa rasmi kumuunga mkono Donald Trump

Rais Barack Obama akimnadi mgombea urais wa Democratic Bi. Hillary Clinton

Rais Barack Obama wa Marekani amewataka viongozi waandamizi wa chama cha Republican kujiondoa rasmi kumuunga mkono, Bw. Donald Trump, kama mgombea wao wa urais.

Katika mkutano wa kumuunga mkono mgombea wa Democratic, Bi. Hillary Clinton, rais Obama amesema ni jambo la busara kutomuunga mkono Trump kwa matamshi yake yenye utata.

Wengi wa wanachama waandamizi wa Republican wametangaza kuto jihusisha tena kumuunga mkono Bw. Trump, baada ya kutolewa kwa video akijitapa kuwa na uwezo wa kuwadhalilisha wanawake atakavyo.

Akiongea kwenye mkutano uliofanyika huko Greensboro, North Carolina, rais Obama amesema huitaji kuwa mume ama baba kusema kuwa alichoongea Trump si sawa, bali unapaswa kuwa muungwana tu kubaini hilo.