Alhamisi , 4th Mei , 2023

Wakazi wa Tabata, Kata ya liwiti mtaa wa mfaume wameitaka serikali kuingilia kati mgogoro wa kuvunjwa kwa ofisi ya serikali ya mtaa wa Mfaume, na kusababisha wananchi kukosa huduma kwa muda wa wiki mbili.

Wakizungumza na EATV wamebainisha kuwa kuvunjwa kwa ofisi hiyo ya serikali ya mtaa wa mfaume usiku wa manane pasipo wananchi kushirikishwa wamesikitishwa na hatua hiyo ukizingatia ofisi hiyo ilijengwa kwa ushirikiano wa wananchi na viongozi wa eneo hilo mwaka 2011.

Pia wananchi hao wameeleza kuwa hawakubaliani na hawajaridhishwa na ofisi mpya ya serikali ya mtaa iliyojengwa na mwekezaji aliyejenga maduka katika eneo la ofisi ya zamani kabla ya kubomolewa, huku wakiwataka viongozi kuondoa baadhi ya nyaraka zilizotelekezwa nje na kuzagaa.

Nae Diwani wa Kata ya Liwiti Alice Mwangoma, ambae amekiri kuwepo kwa mgogoro huo ambapo amewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati hatua zikiendelea kuchukuliwa.