Jumapili , 18th Dec , 2016

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka amesema wabadhirifu mkoani humo waanze kujiandaa kuhama kwa kuwa hatakuwa tayari kufanya nao kazi na kuwatetea kuendelea kurudisha nyuma maendeleo ya wana Njombe.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe - Christopher Olesendeka

Olesendeka amesema katika kipindichake cha uongozi atazingatia zaidi kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuhakikisha maendeleo yanasonga mbele.

Nao watumishi wa mkoa wa Njombe wamesema wataendelea kuchapa kazi pamoja na mkuu wa mkoa huyo huku wakimtakia kila la heri mkuu wa mkoa wa Singida.

Msikilize hapa

Sauti ya Christopher Ole Sendeka
Sauti za wananchi Njombe