
Onyo hilo limetolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Muliro Jumanne, kufuatia kuwepo kwa baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyopelekea kuvuruga uchaguzi wa serikali za mitaa unotarajiwa kufanyika November 24 mwezi huu.
Kwa upande wake mwanaharakati wa kupiga vita vitendo vya kupiga ramli chonganishi mkoani humo Sheikh Mohamed Said, amebainisha kuwa wataalamu wa dawa za kisuna pamoja na waganga wa tiba asili wapo tayari kushirikiana na jeshi hilo kuwafichua wanaopiga ramli chonganishi.
Tazama Video hapo chini kamanda Muliro akieleza jitihada zinazofanywa na jeshi la polisi ili kuwabaini waganga hao.