Jumatano , 20th Jul , 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya awamu ya tano itatoa msukumo mkubwa katika kukabiliana na tatizo la utapiamlo nchini kwa kuweka mipango na mikakati imara ikiwemo kuongeza bajeti ya lish

kuongeza virutubisho kwenye vyakula na kutumia vyema wataalamu wa lishe katika kupambana na tatizo hilo hapa nchini.

Mh. Samia ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Dunia ya Utapiamlo ambayo imetilia mkazo masuala ya lishe kama msingi wa maendeleo hapa nchini na duniani kwa ujumla.

Ameeleza kuwa jitihada zinazofanywa na serikali kwa ushirikiano na wadau wa Maendeleo wa Ndani na Nje ya Nchi zimesaidia kwa kiasi kikubwa kushusha kiwango cha udumavu nchini kutoka 42% mwaka 2010 hadi kufikia 34% mwaka 2015.

Amefafanua kuwa kutokana na mafanikio hayo, serikali imetoa mwongozo wa bajeti ya mwaka 2016/17 kwa kutenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya masuala ya lishe kwa kila mtoto wa umri chini ya miaka mitano hapa nchini.

Naye mkurugenzi wa PANITA Tumaini Mikindo amebainisha kuwa kutokana na ripoti hiyo Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kuwa na watoto wengi wenye utapuia mlo na udumavu hivyo ni vyema kwa wazazi kuhakikisha wanawapa watoto wao vyakula vyenye virutubisho vya muhimu ili kuboresha afya zao