
Pascal Ochiba alikamatwa Januari mwaka huu akiwa na vipande viwili vya pembe za ndovu vyenye uzito wa takriban kilo 10.
Hakimu mkazi wa mahakama hiyo amesema kwamba Bw Ochiba amekua akitenda kosa hilo mara kadhaa na alistahili kifungo cha juu, kwa ajili ya kuwalinda wanyama hao ambao wapo hatarini kutoweka.
Mnamo Julai 2017, Bw Ochiba alikamatwa akiwa na vipande vinne vya pembe za ndovu na ngozi ya okapi na kupelekwa gerezani.
Mwaka 2019, Uganda ilipitisha sheria ya kifungo cha maisha gerezani kwa watu waliopatikana na hatia ya ujangili au usafirishaji haramu wa viumbe walio hatarini kutoweka.
Kuna zaidi ya tembo 7,900 waliosalia porini nchini Uganda, na aina hiyo iko hatarini.