Alhamisi , 13th Oct , 2016

Mkuu wa Kitengo cha Sheria Toka Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Bw. Moses Mbunda amewataka wananchi kupima mitungi ya gesi kabla ya kuinunua kwa matumizi ili kubaini kama kipimo wanachoambiwa ni sawa na mizani itakavyoonesha .

Mitungi ya gesi

Mbunda ameyasema hayo katika kipindi cha EADRIVE kinachorushwa na East Africa Radio wakati akitoa elimu kwa raia kuhusu umuhimu wa kupima gesi kabla ya kuinunua ili kuepuka kulanguliwa.

“Kumeubuka wimbi la wauzaji gesi kutokuwa waaminifu katika kazi zao na mitungi yao inapaswa kuhakikiwa na raia wakati wa manunuzi ili kuepuka kulanguliwa” Amesema Mbunda.

Aidha Mbunda amewataka mawakala wa uuzaji gesi nchini kuhakikisha wanawauzia wananchi bidhaa hiyo kulingana na idadi ya ujazo wanaowaambia ili kuepuusha migogoro isiyo ya lazima katika biashara hiyo.