Jumatano , 9th Sep , 2015

Wagombea ujumbe wa baraza la wawakilishi kutoka vyama vya CCM na CUF wamewekeana pingamizi kupinga uteuzi kwa madai ya udanganyifu,uraia na tuhuma za kesi za kukutwa na silaha zikiibuka.

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mhe Salum Kassim Ali

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Magharibi Suluhu Rashid amesema wilaya ya Magharibi imepokea pingamiizi zipatazo tisa kutoka vyama hivyo viwili ikiwemo ya aliyekuwa waziri katika serikali za awamu zilizopita na kuhamia CUF, Mansour Yussuf Himid amewekea pingamizi na mgombea mwenzake Mwanaisha Khamis kwa madai ya kudanganya kuhusu kesi zake za kukutwa na silaha..

Naye Wakala wa mgombea wa CUF jimbo la Fuoni Ally Saleh amesema madai ya mgombea wa CCM, hayakuwa na uzito wowote kwa vile mgombea huyo amemaliza kidato cha nne na hakudanganya huku mgombea wa CCM, Yussuf Hassan Iddi naye amepinga madai hayo akidai mgombea huyo amedanganya kuhusu elimu.

Pingamizi hizo pia zimemkumba waziri wa Biashara Nassor Mazrui ambaye ni mgombea wa CUF -mtoni na mgombea wa CCM jimbo la Kikwajuni Nasser Salum Aljazira kwa madai ya kuwa na uraia wa nchi mbili.

Hata hivyo tume hiyo ya uchaguzi leo imetangaza kuyatupa mapingamizi yote, na wagombea wote wameruhusiwa kuendelea na kampeni.