Polisi Geita haitambui maandamano BAWACHA

Jumanne , 11th Mei , 2021

Polisi mkoa wa Geita imesema haina taarifa zilizoenea mtandaoni kuhusu maandamano yaliyotangazwa na Baraza la Wanawake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA), mkoa wa Geita.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe

Taarifa hizo zilieleza kuwa BAWACHA wataendesha maandamano kutoka wilayani Chato kuelekea Dodoma, kuhusu kumpinga spika wa Bunge juu wabunge 19 wakuteuliwa ambao hawana chama.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe anasema hana taarifa yeyote kuhusu maandamano hayo hivyo kama wamepanga kufanya hivyo basi wafate taratibu.

Mwenyekiti wa BAWACHA mkoa wa Geita Hellena Thobias na mwenyekiti wa BAWACHA wilaya ya Chato, Husna Saidi wamesema wataendelea na msimamo wao jinsi walivyojipanga kufanya maandamano hayo kuelekea Dodoma.