
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Singida, Mohamedi Likwata, amesema madereva hao wamekamatwa katika operesheni maalumu kwa makosa ya kuendesha mabasi kwa mwendo kasi, huku matairi ya baadhi ya mabasi yakiwa vipara na bila stadi, na vilevile viti vya abiria kukosa mikanda na vioo vya magari mengine vikiwa na nyufa.
Kamanda Likwata amesema wameamua kuwafikisha mahakamani badala ya kuwapiga faini kwa sababu baadhi ya madereva wamekuwa wakifanya makosa ya kuendesha gari kwa mwendo wa kasi kwa makusudi, na pindi wanapokamatwa hulipa faini na kuendelea na mwendo kasi, hivyo kufikishwa mahakamani madereva hao itakuwafundisho kwa madereva wenye tabia hiyo na itasaidia kupunguza ajali ambazo zinagharimu maisha ya abiria.