Jumanne , 26th Jul , 2022

Jeshi la Polisi nchini limetoa onyo kwa baadhi ya madereva wa magari makubwa ya mazigo  wanaohamasisha mgomo wa madereva ili kuzuia magari mengine yasifanye shughuli za usafirishaji kwa kisingizio cha madai ya haki zao wanazodai kutoka kwa waajiri wao kutokuwalipa posho zao

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Awadhi Juma Haji

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Awadhi Juma Haji, amesema kuwa, Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa wanaotumia kisingizio cha mgomo huo kuzuia madereva wengine wasitoe huduma za usafirishaji na kuwataka wafuate taratibu za kisheria.

Aidha, kamishna Awadhi amewaagiza Makamanda wa Polisi wa mikoa kuwachukulia hatua kali za kisheria watu watakaobainika kuhamasisha madereva wenzao kufanya mgomo huo.