Ijumaa , 3rd Feb , 2023

Mahakama nchini Kenya imemhukumu kifo polisi wa zamani wa Kenya kwa mauaji ya wakili maarufu wa haki za binadamu na watu wengine wawili zaidi ya miaka sita iliyopita.

Marehemu Wakili Willie Kimani

 

Polisi wengine wawili wa zamani na raia walihukumiwa kifungo cha kati ya miaka 20 na 30 jela kwa mauaji ya wakili Willie Kimani, mteja wake na dereva wa teksi mnamo Juni 2016.

Wanne hao walipatikana na hatia ya makosa matatu, likiwemo la mauaji, Julai 2022.Hukumu ya kifo kwa mauaji nchini Kenya hubadilishwa na kuwa kifungo cha maisha jela.

 Hata hivyo, uamuzi wa Mahakama Kuu wa mwaka 2017 uliwapa majaji busara ya kuamua ikiwa hukumu ya kifo bado inaweza kutolewa.Afisa wa jeshi aliyehusika na jaribio la mapinduzi mwaka 1982 alikuwa mtu wa mwisho kunyongwa nchini Kenya.

 Mauaji ya Kimani yaliangazia mauaji mengi ya kiholela na kutoweka ambayo yamekuwa yakilaumiwa kwa polisi wa Kenya.

Afisa wa zamani wa polisi Fredrick Leliman, ambaye alihukumiwa kifo, na washtakiwa wengine watatu, wanaweza kukata rufaa dhidi ya kutiwa hatiani na kuhukumiwa ndani ya siku 14.