Ijumaa , 12th Jun , 2020

Jeshi la Polisi nchini limesema upelelezi wa tukio la kushambuliwa kwa M/kiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, limebaini kuwa eneo la tukio kulikuwa na watu ambao wangeweza kusikia lakini hawakuona tukio lolote na hata alipofikishwa Hospitali alikuwa kalewa chakari na kushindwa kutamka maneno.

Kulia ni Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime na kulia ni M/Kiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi hilo SACP David Misime, na kuongeza kuwa  kwa mujibu wa maelezo ya Mbowe alisema kuwa tukio hilo lilimpata majira ya saa 7 usiku, wakati akitokea kwa mzazi mwenzake Joyce Mukya, na hata baada ya tukio kutokea walimpigia yeye na hakuona umuhimu wa kupiga simu Polisi.

"Uchunguzi wetu umethibitisha kuwa siku ya Juni 8, 2020, Mbowe alitembelea sehemu kadhaa za starehe zinazouza vileo ikiwemo Royal Village, na kupata kilevi na hata alipofika hospitalini alionekana akiwa kwenye hali ya ulevi chakari, kiasi cha kushindwa kutamka maneno sawa sawa" amesema SACP Misime.

Aidha ameongeza kuwa "Upelelezi wetu umepata ushahidi wa kutosha kutoka kwenye eneo la tukio unaoonesha kuwa kulikuwa na watu ambao kwa namna yoyote, wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada, lakini kwa mujibu wa mashahidi hakuna hata mmoja aliyeweza kusikia kelele wala kuona tukio la Mbowe kushambuliwa".

Tazama video hapa chini.