Jumanne , 19th Sep , 2023

Jeshi la Polisi nchini linamsaka mtu aliyemfanyia kitendo cha ukatili na udhalilishaji mtoto mdogo kwa kumfunga kamba akiwa mtupu na kisha kumning'iniza, ambapo limeombayeyote anayejua mahali kitendo hicho kilipofanyika atoe taarifa ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Mtoto

 

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini SACP David Misime amesema kwamba walianza kuifanyia kazi video hiyo tangu ilipoanza kusambaa mitandaoni na hivyo kwa yeyote anayejua aliyefanya ukatili huo atoe taarifa ili asaidie kukamatwa kwa mhusika.