Jumatano , 21st Jul , 2021

Kongamano la Chama cha Siasa cha CHADEMA la kudai Katiba mpya lililokuwa lifanyike leo Jijini Mwanza, limeshindwa kufanyika baada ya polisi waliobeba mabomu ya machozi, silaha za moto pamoja na magari yenye mbwa kutanda katika eneo la hoteli mahali ambapo kongamano hilo lingefanyika.

Mbwa na Polisi waliozuia kongamano la CHADEMA Mwanza

Hapo jana Julai 20, 2021, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel, alipiga marufuku mikusanyiko isiyo ya lazima katika mkoa huo kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa hatari wa Corona.

Hadi EATV inaondoka katika eneo hilo jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng’anzi, ziligonga mwamba baada ya kupigiwa simu mara kadhaa na kutopokea, lakini hivi karibuni RPC huyo alisema hatoruhusu kufanyika kwa mikutano isiyokuwa na vibali.