Polisi yamsaka aliyeua mtoto kisa njiwa

Alhamisi , 22nd Nov , 2018

Jeshi la Polisi mkoani Manyara linamtafuta kijana aliyefahamka kwa jina la Aman Filipo kwa tuhumza kusababisha kifo cha mtoto wa miaka 11 Emanueli Justine baada ya mtoto huyo kusadikika kuiba njiwa wake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa Manyara Augustine Senga.

Akizungumza na www.eatv.tv, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Augustine Senga, amesema kwa hatua ya awali Jeshi hilo linamshikilia mama mzazi wa mtoto huyo kwa madai ya kushiriki kifo cha mwanaye wakati akiadhiabiwa na mtuhumiwa, kijana Aman Philipo.

Tunamshikilia mama mzazi wa mtoto aliyefariki, Mariamu Daudi kwa kushuhudia na kuruhusu mtoto wake kupigwa na Aman Filipo kwa madai ya kuiba njiwa na kupelekea kifo cha mtoto huyo baada ya kupewa adhabu kupita kiasi,” amesema Kamanda Asenga.

Kwa taarifa tulizopata, kijana aliyefanya unyama huo anajulikana katika mtaa wake hivyo tunaendelea kufanya upelelezi na tukimkamata hatua zingine zitaendelea za kuwafikisha watuhumiwa mahakamani kwa ajili ya kujibu mashtaka," ameongeza Senga.

Aidha Kamanda Senga ameitaka Jamii kutumia madawati mbalimbali ya yanayojihusisha na masuala ya watoto ili kujua namna ya kuyakabili matatizo ya watoto.

 

Kusikia alichozungumza Kamanda wa Polisi Manyara Agustino Senga bonyeza link hapo chini