Jumanne , 17th Apr , 2018

Mjukuu wa Malkia Elizabeth wa Uingereza, William Arthur amemuahidi Makamu wa Rais Samia Suluhu kuwa ataisaidia Tanzania katika kuboresha ulinzi wa wanyama pori kwa kutumia teknolojia ya hali juu na kumualika Rais Magufuli katika mkutano wa masuala ya wanyapori utakaofanyika Oktoba 2018.

Prince William ameeleza hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mama Samia leo katika Jumba la Kifalme la Buckingham Palace nchini Uingereza ambapo Makamu wa Rais amekwenda kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa nchi za jumuiya ya Madola.​

Kwa upande wake Makamu wa Rais alimweleza Prince William kuwa Tanzania inatambua mchango wake katika kuzuia ujangili wa wanyama pori na serikali ya Tanzania imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ya kupambana na kuzuia ujangili ingawa bado haijawa na teknolojia yenye uwezo wa wa kutambua na kuona wanyama wote lakini wameendelea kuimarisha ulinzi wa wanyama pori.

Mtazame hapa chini Makamu wa Rais Samia Suluhu akiwa anazungumza na Prince William