Jumanne , 12th Aug , 2025

Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin wanatarajia kukutana ijumaa hii kujadili namna ya kumaliza mzozo wa Urusi na Ukraine

Rais wa Marekani Donald Trump amesema atautumia mkutano unaotarajiwa kati yake na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kupima fikira za Putin kumaliza mzozo wa Ukraine.

Trump amemkaribisha mwenzake wa Urusi nchini Marekani Ijumaa ya wiki hii kwa mkutano wa moja kwa moja kati ya viongozi wa mataifa hayo mawili tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwezi Februari mwaka wa 2022.

Trump amezungumzia mkutano huo wakati huu pia akimtuhumu mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa kukataa mapendekezo ya kuachia baadhi ya maeneo nchini mwake wa Urusi.

Kutokana na hofu kwamba Trump anaweza kukubaliana na Putin kuhusu suala la Ukraine, viongozi wa Umoja wa Ulaya nao wanapanga kuwa na mazungumzo kati ya Trump na Zelensky kwa nyakati tofauti.

Rais wa Marekani alitumia miezi zake za kwanza za awamu yake ya pili Ofisini kujaribu kupata suluhu ya kupata mwafaka kati ya Ukraine na Urusi.
Trump alikuwa ameahidi kumaliza vita vya Ukraine katika muda wa saa 24, mazungumzo kadhaa pamoja na ziara ya kidiplomasia zikishindwa kuzaa matunda.