Alhamisi , 25th Jun , 2015

Watu watatu raia wa Kenya wamekamatwa kwa kujiandikasha katika daftari la wapiga kura wilayani Bunda mkoani Mara.

Raia wa Kenya waliokamatwa

Jeshi la polisi kwa kushirikiana na idara ya uhamiaji wilayani Bunda mkoani Mara limewakamata watu watatu raia wa nchi jirani ya Kenya kwa kosa la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kinyume cha sheria.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bunda bw Joshua Mirumbe, ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Bunda, ameiambia EATV mjini Bunda kuwa watu hao walijiandikisha kwa lengo la kutaka kupiga kura nchini kinyume cha sheria za nchi.

Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya ya Bunda amewataka wananchi kujitokeza katika zoezi la uandikishaji linaloendelea na kutoa onyo kali kwa baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakifanya fujo katika maeneo ya vituo huku wegine wakishinikisha kuandikishwa zaidi ya mara moja.