Jumatano , 6th Dec , 2023

Jarida maarufu la TIME kutokea nchini Marekani, limemtaja mchezaji wa klabu ya Inter Miami na timu ya taifa ya Argentina Leo Messi. kama mwanamichezo bora wa mwaka.

 

Ubora wa Leo Messi umetambulika baada ya ushawishi mkubwa kwenye upande wa michezo nchini Marekani, baada ya kuhamia kwenye klabu ya Inter Miami.

 

Kufanikisha timu yake ya taifa kunyakua kombe la Dunia mwaka 2022, zaidi ya hayo kuchukua tuzo ya 8 ya Ballon d'Or

 

Hii ni kudhihirisha ubora na umahiri wa mchezaji huyo kwenye upande wa michezo

 

Picha: Messi