Jumatatu , 17th Aug , 2015

Waziri wa Nishati na Madini Mh. George Simbachawene ameuagiza uongozi wa Kampuni ya Tanzanite One ya Mjini Arusha uwatimue kazi raia 30 wa kigeni waliajiriwa katika kampuni hiyo kama wataalamu.

Waziri wa Nishati na Madini, Mh. George Simbachawene

Simbachaene amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizindua kamati ya pamoja ya uendeshaji ya mgodi wa Tanzanite na kati ya serikali yenye wajumbe sita wakiwemo watatu kutoka serikalini.

Mh. Simbachawene amesema inashangaza kuona raia kutoka Asia wakiwemo wahindi zaidi ya 52 wameajiriwa kufanya kazi katika mgodi wa Tanzanite One wakati kazi hiyo inaweza kufanywa na raia wa Tanzania.

Aidha waziri huyo aliitaka kampuni hiyo kuhakikisha inaboresha huduma mbalimbali za wafanyakazi na kutekeleza kwa vitendo ahadi zote walizoahidi baada ya kusaini mkataba wa kununua hisa asilimia 50.